Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imeendelea kujidhihirisha kama moja ya nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi barani Afrika huku mfumuko wa bei ukibaki katika kiwango thabiti cha asilimia 3.3, na deni la Taifa likiendelea kuwa himilivu hali inayojenga imani ya wawekezaji na taasisi za kimataifa.
Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akishiriki sherehe za mwaka mpya wa Mabalozi pamoja na mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania, ambayo imefanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma na kuwahakikishia mageuzi ya misingi ya kiuchumi ikiwemo upungufu wa fedha za kigeni, uimarishaji wa uwiano wa kodi za pato la taifa pamoja na mageuzi ya utawala bora.
Mbali na hilo amebainisha juu ya Tanzania kuunganisha rasilimali zake kuhakikisha zinachangia maendeleo ya teknolojia na ukuaji jumuishi huku miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo SGR na bomba la mafuta la Afrika Mashariki, inaendelea kwa kasi na ni msingi wa kufungua uchumi wa Taifa.
Kwa upande wa diplomasia, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabiti Kombo amesema hatua hizi zimewezesha Tanzania kudumisha kasi ya maendeleo, kuimarisha mahusiano ya pande mbili na kushirikiana kwa heshima na washirika wa kikanda na kimataifa.
Chanzo; Clouds Media