Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam imepanga kesho Oktoba 7, 2025 kuendelea na ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ambaye kesho anatarajiwa kumuhoji maswali ya dodosi (cross examination) Shahidi wa kwanza wa Jamhuri ambaye ni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) George Bagyemu ambaye leo alitoa ushahidi wake Mahakamani hapo.
Nje ya Mahakama, Wakili Gaston Shundo Garubindi ambaye ni Mkurugenzi wa Sheria wa CHADEMA amenukuliwa akieleza yafuatayo "leo Jamhuri wameleta Shahidi mmoja tangu asubuhi tumemsikiliza Shahidi wao mpaka sasa tunapoahirisha shauri hili, tunaendelea kesho kwa kumpa fursa Mwenyekiti ambaye atakuwa na nafasi ya kumuhoji maswali ya dodoso kuhusu kile alichokisema na mambo mengine”
Chanzo: Millard Ayo