Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Uber Yajiondoa Tanzania Moja kwa Moja

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini ( LATRA ), imeeleza kuwa imepokea barua kutoka Ofisi za UBER zilizopo Amsterdam, Uholanzi na kuthibitisha kuwa ni kweli Kampuni hiyo ya Taxi Mtandao ya Kimataifa imesitisha shughuli zake Nchini Tanzania.

Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano ( LATRA ) Salum Pazi kwenye mahojiano maalum na Ayo Tv, amesema UBER wamesitisha kwa muda huduma zao kuanzia Jumamosi January 31 2026 na kwamba hawajajiondoa moja kwa moja kufanya biashara Nchini Tanzania.

"Barua hiyo imetutaarifu rasmi kwamba Kampuni ya UBER inasitisha kwa muda na hapa napenda nieleze vizuri sio kwamba imesimamisha kabisa au imejiondoa moja kwa moja, imesitisha kwa muda wametumia neno ku-PAUSE badala ya ku-END, kwamba wamesitisha kwa muda biashara zao na sababu ni kutokana na changamoto walizokutana nazo katika uendeshaji wa shughuli zao hapa Nchini" - Salum Pazi.

"Tunapenda kuwajulisha Watanzania na Wadau wote kwa ujumla kwamba kwakuwa wamesitisha kwa muda hali hii ni ya kawaida ambayo huwa inajitokeza kwa Kampuni mbalimbali , tunataraji katika siku za usoni huenda tukawa nao tena nadhani mnafahamu sio mara ya kwanza jambo hili kutokea hawahawa UBER miaka ya nyuma walishawahi pia kusitisha na baadae wakarejea" - ameeleza Salum Pazi. 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: