Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ajira 20,000 Kutororewa Mradi wa Dhahabu Kigosi

Wananchi wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wanatarajiwa kunufaika na ajira takribani 20,000 pamoja na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi kutokana na uwekezaji unaotarajiwa kuanza katika eneo la madini ya dhahabu Kigosi.

Mradi huo pia unatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali pamoja na kuleta teknolojia ya kisasa katika sekta ya madini.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa uwekezaji kati ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na kampuni ya Plantcor Mining and Plant Hire (Pty) Ltd, Naibu Waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa amesema uwekezaji huo ni hatua muhimu katika kuendeleza rasilimali za madini na kukuza uchumi wa taifa.

“Mradi huo unatekelezwa kwa mfumo wa ubia. STAMICO, kwa niaba ya serikali ya Tanzania, itashiriki katika hatua zote muhimu kuanzia utafiti wa kina wa madini, uendelezaji wa mgodi hadi uzalishaji.

“Muundo huo unalenga kulinda maslahi ya taifa huku ukiwezesha upatikanaji wa teknolojia na utaalamu wa kisasa kutoka kwa wawekezaji wa kimataifa,” amesema Dk. Kiruswa.

Aidha Mwakilishi wa Kampuni ya Plantcor nchini Tanzania Deogratius Kumalija akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo amesema uwekezaji huo unatarajiwa kuongeza ajira kwa Watanzania, kuongeza mapato ya serikali na kuleta teknolojia ya kisasa katika sekta ya madini.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: