Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Nizhny Novrogod Yaitika World Youth Festival Assembly

Mamia ya vijana toka Urusi na mataifa mbalimbali duniani wamejitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kongamano la Dunia la Vijana (World Youth Festival 2025) linalofanyika Niznhy Novrogod, nchini Urusi. Kongamano hilo linalofanyika kwa siku 5 mfululizo kuanzia leo Septemba 17 limeweza kuibadilisha mandhari ya jiji la Niznhy Novgorod ndani na je ya ukumbi ambapo mitaani kote kuna mabango yanayoashiria tukio hili kubwa huku uwepo wa mchanganyiko wa vijana wa nchi tofauti ukiashiria uwe wa ugeni mkubwa katika jiji hili.

Shamrashamra za ufunguzi huo zimepambwa na matukio mbalimbali ya kiburudani yaliyofanyika katika eneo la ukumbi ambapo shughuli tofauti za kuonyesha utamaduni wa Urusi katika nyanja tofauti zimefanyika na kushuhudiwa na wahudhuriaji waliojitokeza. Burudani hizo zimegawanyika katika maeneo tofauti ya ndani ya eneo la tukio ambapo majukwaa yamajengwa ili kutoa ladha tofauti za utamaduni kwa wahudhuriaji ikilenga kuonyesha historia, mila na desturi za Urusi ambayo ni moja ya mataifa kongwe duniani yaliyoweza kustaarabika mapema na kuhamasisha utamaduni wake kusambaa maeneo mengine.

Katika hatua nyingine vijana washiriki wamepata fursa ya kutembezwa maeneo mbalimbali ya vivutio katika jiji la Niznhy Novrogod ili kujifunza historia, mila na utamaduni wake. Ziara za kujifunza zimesimamiwa na vijana wa kujitolea (volunteers) toka katika jiji la Nizhny Novgorod na mikoa mingine 54 ya Urusi wakisaidia kutoa huduma katika maeneo tisa tofauti ikiwa ni pamoja na usafiri, utoaji habari, utoaji vibali, kusimamia eneo la tukio, itifaki, huduma za kijamii, kusimamia programu, huduma ya lugha na utoaji taarifa.

Kongamano hilo litakalofanyika kwa siku 5 mfululizo limewakutanisha vijana 2000 toka mataifa 120 likilenga kufungua ushirikiano baina ya vijana duniani kote ambapo kwa mwaka huu zaidi ya maombi 62000 yalipokelewa na kisha mchujo wa kupatikana kwa waliohudhuria ukifanyika.

Kongamano la Vijana Duniani linaandaliwa na Shirikisho la Masuala ya Vijana (Rosmolodezh), kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Niznhy Novgorod na kuendeshwa na World Youth Festival Directorate ambapo Clouds Media pia ina uwakilishi wake kupitia kwa mtangazaji wa kipindi cha Sentro, Ally Kashmiry na Mkuu wa Kitengo cha Digital Shafii Mpanja.

Kuhusiana na mada hii: