Tawi la kundi la kigaidi linalojiita dola la kiislamu IS limedai kuhusika na shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya msikiti mmoja wa madhehebu ya Washia Pakistan lililosababisha vifo vya watu 31 na kujeruhiwa kwa wengine 169, huku waombolezaji wakikusanyika leo chini ya ulinzi mkali katika msikiti huo huo kwa mazishi ya waathiriwa.
Katika taarifa iliyochapishwa katika shirika la habari la Amaq, tawi hilo linajulikana kama IS Pakistan, lilidai kuhusika katika shambulizi hilo.
Inasema mshambuliaji huyo aliwafyatulia risasi walinzi waliojaribu kumzuia kwenye lango kuu la msikiti huo na kulipua bomu alilokuwa amelivaa mwilini katika lango la ndani.
Chanzo; Dw