Maafisa wa Denmark na Greeland wamesema wameshindwa kuafikiana na kubadili mawazo ya utawala wa Rais Donald Trump kuhusu azma ya Marekani kukinyakua kisiwa kinachojitawala cha Greenland.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Lars Lokke Rasmussen na mwenzake wa Greenland Vivian Motzfeldt walikutana jana na Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio.
Chanzo; Dw