Waziri wa zamani wa Kilimo wa Nchini China Tang Renjian amehukumiwa kifo baada ya Mahakama kumkuta na hatia ya kula rushwa ya pesa za China ambazo ni sawa na Tsh. milioni 92 za Tanzania.
Imeelezwa kuwa Waziri huyo wa zamani alichukua hongo ya mali pamoja na pesa taslimu katika nyadhifa mbalimbali alizoshikilia kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2024 ambapo hata hivyo Mahakama imeahirisha hukumu yake ya kifo kwa miaka miwili kutokana na kitendo chake cha kukiri makosa yake.
Chama cha Kikomunisti cha China kilimuondoa Tang kwenye Uongozi tangu Novemba 2024 ikiwa ni miezi sita baada ya kuwekwa chini ya uchunguzi na Shirika linalopinga ufisadi.
Chanzo; Millard Ayo