Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Iran Yarejesha Mabalozi Nyumbani

Iran imewarejesha nyumbani mabalozi wake katika nchi za Ujerumani, Ufaransa na Uingereza. Shirika la habari la Mehr la Iran limeripoti leo Jumamosi kuwa mabalozi hao wamerudishwa nyumbani ili kufanya mashauriano kuhusu mgogoro wa mchakato wa Umoja wa Mataifa ulioanzishwa na nchi hizo wa kuirejeshea tena vikwazo Tehran.

Jana Ijumaa, juhudi za Urusi na China za kuchelewesha kufufua vikwazo dhidi ya Urusi ziligonga mwamba mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Hayo yanajiri wakati Umoja wa Mataifa ukitazamiwa kuiwekea vikwazo vikali Iran leo Jumamosi baada ya mazungumzo ya nyuklia kati ya taifa hilo na mataifa ya magharibi kukwama. Vikwazo hivyo vitakapotangazwa vinatazamiwa kuanza kufanya kazi kuanzia siku ya Jumapili.

 

Chanzo: Dw

Kuhusiana na mada hii: