Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetangaza kusitishwa kwa utoaji wa viza karibu zote kwa raia wa Tanzania kuanzia Januari 1, 2026, kufuatia Tamko la Rais Na. 10998.
Kwa mujibu wa tamko hilo, viza za kutembelea (B1/B2), masomo na mabadilishano (F, M, J), pamoja na viza zote za uhamiaji hazitatolewa tena kwa Watanzania, isipokuwa katika mazingira machache maalumu kama uraia pacha, wakaazi halali wa kudumu wa Marekani (Green Card holders), viza maalum za wafanyakazi wa serikali ya Marekani, na washiriki wa mashindano makubwa ya michezo.
Ubalozi umeeleza kuwa viza zilizotolewa kabla ya Januari 1, 2026 hazitafutwa, lakini Watanzania wataendelea kukumbwa na vikwazo vikubwa vya kuingia Marekani hata kama wataomba au kuhudhuria usaili.
Hatua hii imezua mshangao na maswali mazito kuhusu mustakabali wa mahusiano ya Tanzania na Marekani, pamoja na athari kwa wanafunzi, wafanyabiashara na familia zilizo na uhusiano wa kimataifa.
Chanzo; Cnn