Idadi ya vifo yazidi kuongezeka Ufilipino kufikia 27 na majeruhi zaidi ya 140 kutokana na tetemeko la ardhi lilitokea mapema wiki hii.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters idadi vifo inaweza kuongezeka kadri maafisa uokoji wanavyozidi kuuafikia majengo yaliyoporomoka.
Ambapo, Tetemeko hilo lilitokea pwani ya Mji wa Bogo katika Mkoa wa Cebu, eneo la Visayas la kati, kabla ya saa nne usiku Jumanne September 31,2025 na kusababisha kukatika kwa umeme na kuangusha majengo, likiwemo kanisa kongwe la miaka 100.
Cebu, moja ya miji inayovutia watalii zaidi nchini Ufilipino, wenye wakazi milioni 3.4 na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mactan-Cebu, ambao ni wa pili kwa uchukuzi nchini humo, ulibaki wazi.
Tetemeko hilo lilitokea zaidi kaskazini mwa Cebu na San Remigio, miji ambayo ilitangazwa kupatwa kwa maafa ili kurahisisha jitihada za utoaji misaada na uokoaji.
Alfie Reynes, makamu meya wa San Remigio, aliomba chakula na maji kwa waliokimbia makazi yao, pamoja na vifaa vya kuokoa vinavyohitajika na wafanyakazi wa uokoaji.
"Mvua inanyesha kwa kiasi kikubwa na hakuna umeme, kwa hivyo tunahitaji msaada, hasa kaskazini kwa sababu kuna uhaba wa maji baada ya mabomba kuharibiwa na tetemeko," - Reynes
Chanzo: Tanzania Journal