Rais wa Madagascar Andry Rajoelina ameivunja serikali yake jana Jumatatu baada ya siku kadhaa za machafuko makubwa ambayo Umoja wa Mataifa umesema yalisababisha vifo vya watu 22.
Rajoelina alisema alipolihutubia taifa kwa njia ya televisheni kwamba ameamua kusitisha shughuli za Waziri Mkuu na serikali na kuongeza kuwa Waziri Mkuu huyo Christian Ntsay na mawaziri wengine watabakia kwa muda hadi serikali mpya itakapoundwa. Ametoa siku tatu za kupendekeza Waziri mkuu mpya.
Chanzo: Dw