Kijana mmoja wa jimbo la Florida anakabiliwa na mashtaka mazito ya jinai (felony) baada ya kudaiwa kumuunguza rafiki yake kwa moto na tukio hilo lililonaswa kwa video na kusambaa kwa kasi mitandaoni.
Kwa mujibu wa mamlaka za usalama tukio hilo lilitokea wakati vijana hao walipokuwa pamoja na mtuhumiwa anadaiwa kutumia moto kumchoma na kusababisha rafiki yake kupata majeraha makubwa.
Polisi wamethibitisha kuwa mtuhumiwa amekamatwa na kufikishwa mahakamani na uchunguzi ukiendelea kubaini mazingira kamili ya tukio hilo na hali ya majeruhi inaendelea kufuatiliwa na madaktari.
Tukio hilo limeibua wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa vijana na vitendo hatarishi huku mamlaka zikitoa wito kwa jamii kuzingatia sheria na kulinda maisha ya wenzao.
Chanzo; Bongo 5