Idara ya Afya ya Jiji la New York nchini Marekani imetoa orodha ya majina ya watoto maarufu zaidi kwa 2024, huku majina ya Mia na Noah yakitajwa kuongoza orodha hiyo kwa kuwa na watoto wengi wakike na wakiume.
Kati ya watoto 65,222 waliozaliwa katika jiji hilo mwaka jana, watoto 722 wamepewa jina la Noah na watoto 422 wamepewa jina la Mia, majina haya yameyapiku Liam na Emma, ambao walikuwa wanaongoza orodha hiyo tangu 2016 na 2017.

Kaimu Kamishna wa Afya wa jiji la New York Dk. Michelle Morse amesema orodha hiyo inaangazia kizazi kijacho cha jiji la New York kitakavyokuwa sambamba na kuangazia maisha ya watoto wenye afya katika jiji hilo.
Chanzo; Crown Media