Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Waliokula Mchana Wakamatwa

Polisi wa Kiislamu katika jimbo la Kano kaskazini mwa Nigeria, wanaojulikana kama Hisbah, wamewakamata Waislamu tisa- wanaume saba na wanawake wawili kwa kosa la kula chakula hadharani siku ya kwanza ya mfungo wa Ramadhani.

Mwezi wa Ramadhani umeanza nchini Nigeria siku ya Jumatano, Februari 18, 2026. Kwa mujibu wa sheria za Sharia zinazotumika katika majimbo 12 ya kaskazini mwa nchi hiyo, Waislamu wote wenye uwezo wanapaswa kufunga kuanzia kuchomoza kwa jua hadi kuzama kwake.

Naibu Kamanda Mkuu wa Hisbah, Mujahid Aminudeen, ameiambia BBC kuwa watuhumiwa hao walidai kutojua kuwa mwezi wa Ramadhani umeanza.

Amesema kuwa jeshi hilo halitawapa adhabu kali mara moja, bali litawashikilia kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya kiroho.

Ingawa Kano KUN mfumo wa Sharia, sheria za kiserikali bado zinatumika, na migahawa katika maeneo yenye Wakristo wengi inaruhusiwa kubaki wazi.\

Hata hivyo, Hisbah hufanya doria kila mwaka kuhakikisha Waislamu wanazingatia nguzo hii ya nne ya Uislamu. Mara nyingi, waliokamatwa huachiwa baada ya familia zao kuahidi kuwasimamia ili wakamilishe mfungo wa mwezi mzima.

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: