Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amesema taifa lake lenye silaha za nyuklia linaweza “kuiangamiza kabisa” Korea Kusini endapo usalama wake utatishiwa.
Ametoa kauli hiyo wakati akihitimisha mkutano wa chama tawala ulioweka malengo ya miaka mitano ijayo.
Ameitaja Korea Kusini kuwa adui wa kudumu na kukataa mazungumzo, huku akiacha wazi uwezekano wa majadiliano na Marekani.
Chanzo; Dw