Saudi Arabia imetangaza mabadiliko makubwa ya sera, ikithibitisha kuwa raia wa kigeni wataruhusiwa kununua mali isiyohamishika nchini humo kuanzia mwaka 2026.
Hatua hii inaashiria mara ya kwanza kwa Saudi Arabia kufungua umiliki wa mali kwa wasio raia wa Saudi, na ni sehemu ya mageuzi mapana ya Dira ya 2030 yanayolenga kuvutia uwekezaji wa kigeni na kuupanua uchumi.
Sera hiyo itawahusu wageni kutoka kote duniani, wakiwemo Waafrika, ingawa umiliki utaruhusiwa katika maeneo maalum pekee, huku kanuni na masharti zaidi yakitarajiwa kutolewa na mamlaka husika.
Chanzo; Bongo 5