Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Trump Afuta Video ya Sokwe ya Obama, Mkewe

Rais wa Marekani, Donald Trump, amefuta video yenye kipande cha ubaguzi wa rangi alichochapisha kwenye mitandao ya kijamii kilichomlinganisha Rais wa Zamani, Barack Obama na mkewe Michelle Obama na sokwe.

Hata hivyo, kwa mujibu wa NBC News Trump amesema hataomba msamaha kwa kuchapisha video hiyo.

Video hiyo, yenye muda wa takribani dakika moja, ilihusu madai ya udanganyifu kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, lakini mwishoni ilionesha sura za familia hiyo ya Obama zilizopachikwa juu ya vichwa vya sokwe huku wimbo wa “The Lion Sleeps Tonight” ukipigwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa usiku, Trump alisema:

“Bila shaka nakataa sehemu za ubaguzi wa rangi za video hii, lakini sina mpango wa kuomba msamaha.”

Awali, Ikulu ya Marekani ilijitetea kwa kusema video hiyo ilitoka kwenye video ya vichekesho vya mtandaoni 'meme' lakini baada ya kupokelewa kwa hasira kutoka kwa wanaharakati na baadhi ya wanasiasa wakiwemo wa chama chake, video hiyo ilifutwa.

Msemaji wa Ikulu alisema:
“Mfanyakazi mmoja wa Ikulu kwa bahati mbaya alichapisha video hiyo. Tayari imefutwa.”

Trump hakujibu moja kwa moja Ijumaa usiku kuhusu ni mfanyakazi gani alichapisha video hiyo au kama atafutwa kazi.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: