Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Urusi Yatoa Somo la Kukabiliana na Taarifa Potofu Mitandaoni

 

Kukiwa na ongezeko la taarifa potofu ikiwemo propaganda ambapo kwa kiasi kikubwa ikichangiwa na matumizi mabaya ya Akili Unde (AI), Urusi imetoa somo la namna ya kukabiliana na taarifa hizo.

Akizungumza katika Kongamano la Dunia la Vijana (World Youth Festival Assembly linalofanyika Niznhy Novgorod Urusi, wakati mada maalum inayohusu Matarajio ya Maudhui  ya Vyombo Vya Habari Kufikia Mwaka 2030 (Media 2030: The Future of Content), Mikhail Zvinchuk ambaye ni Mkuu wa Russian Rybar Think Tank amesema ni wakati wa sasa mataifa mengine duniani kuangalia mfano wa Urusi na kutengeneza mpangokazi wa maudhui yanayokabiliana na upotoshaji wa mataifa au watu wenye nia mbaya. 

“Mfano tulipoanza oparesheni maalum ya kijeshi (Ukraine) tuligundua taarifa zinazotengenezwa na washindani wetu wa mataifa mengine zilikuwa ni propaganda zilizotumia ubinadamu, hata hivyo watu wetu walianza kutumia mfumo kama wa Telegram kuelezana ukweli wa kile kinachotokea, hivi sasa Telegram sio kwamba imebaki kuwa sehemu ya kuelezea ukweli kuhusu Urusi, imegeuka kuwa sehemu ywa watu wasioogopa kuhojiana na kwa sasa watu wa mataifa mengine wanajiunga na Telegram na kuitumia kuelezea kile kisichozunguzwa na vyombo vya propaganda”, amesema Zvinchunk.

Ameongeza kuwa kwa sasa ni rahisi kwa watu kudanganyika kwani mitandao inatumia mfumo wa algorithm na kuwalisha kile wanachotaka kukisikia hivyo kuwapunguzia tabia ya kuhoji vitu visivyoendana na imani zao. 

“Unapokabiliana na adui anaetumia propaganda na anamiliki mfumo (algorithm) njia ya kwanza ni kutafuta ni udhaifu wa hoja zake na kumtangulia kutoa majibu yatakayoingia kwenye algorith, lazima ujiulize maswali hayo kabla yake”, ameongeza Zvichunk.

Awali akichangia mada hiyo, Craig Wing, Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Whattheforesight ameeleza kuwa Akili Unde (AI) kwa sasa imetengenezwa bila kuwa na mfumo wa kumlinda mtumiaji hivyo amewataka watu kutosoma maudhui hayo bila kuhoji na kutafuta mawazo tofauti na kile wanachoambiwa na AI.

Kongamano la Vijana Duniani linaandaliwa na Shirikisho la Masuala ya Vijana (Rosmolodezh), kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Niznhy Novgorod limeendelea kwa siku ya pili likiwakutanisha vijana 2000 toka mataifa mbalimbali likilenga kufungua ushirikiano baina ya vijana duniani kote ambapo mada mbalimbali kuhusu ujasiriamali, ubunifu, vyombo vya habari na masuala ya kijamii vimeendelea kuwa sehemu kubwa ya mjadala.

 

Kuhusiana na mada hii: