Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kagame Mpango wa Kumrithisha Mwanae Madaraka

Rais Paul Kagame wa Rwanda amepuuzilia mbali fununu kwamba anamwandaa binti yake Ange Ingabire kuwa mrithi wa kiti cha Rais.

Hayo yameripotiwa na vyombo kadhaa vya habari vya kanda hiyo vikimnukuu Kagame aliyetoa matamshi hayo wakati wa kikao kimoja na maafisa wa serikali mjini Kigali. Amesema ameamua kuweka wazi jambo hilo kwa sababu kwa muda mrefu sasa, uvumi umekuwa ukienezwa kwamba anamsafishia njia binti yake huyo kumrithi.

Kiongozi huyo anayeitawala Rwanda tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, amesisitiza watoto wake wote, kama ilivyo kwa Wanyarwanda wengine wataishi maisha ya kawaida bila upendeleo.

Binti yake, Ange Ingabire Kagame hivi sasa ni naibu mkurugenzi mtendaji wa Baraza la Taifa la Sera na Mipango lililo chini ya Ofisi ya Rais. Kuteuliwa kwake kwenye nafasi hiyo Agosti 2023 kulizidisha uvumi kwamba anaandaliwa kuchukua kiti cha baba yake atakapostaafu.

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: