Mjumbe wa Marekani, Steve Witkoff ametangaza kuanza kwa awamu ya pili ya mpango wa Rais Donald Trump wa kukomesha vita Gaza, huku serikali ya Palestina yenye kuendeshwa na wataalam ikianzishwa katika eneo hilo.
Chini ya awamu ya kwanza, Hamas na Israel zilikubaliana kusitisha mapigano mnamo Oktoba, 2025 pamoja na kubadilishana mateka na wafungwa, kujiondoa kwa kiasi fulani kwa Israel, na ongezeko la misaada.
Witkoff alisema awamu ya pili pia itajumuisha ujenzi mpya na kuondolewa kabisa kwa wanajeshi wa Gaza, ikiwa ni pamoja na kupokonywa silaha kwa kundi la Hamas na makundi mengine ya Wapalestina.
"Marekani inatarajia Hamas kutekeleza kikamilifu majukumu yake," alionya, akibainisha kuwa haya ni pamoja na kurejeshwa kwa mwili wa mateka wa mwisho wa Israeli aliyefariki dunia.
"Kushindwa kufanya hivyo kutasababisha athari mbaya," alisema.
Hata hivyo, mambo mawili muhimu ya awamu ya pili yanaweza kuwa changamoto.
Hamas hapo awali ilikataa kuachana na silaha zake kabla ya kuundwa kwa taifa huru la Palestina, na Israeli haijajitolea kujiondoa kikamilifu Gaza.
Chanzo; Global Publishers