Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Bilionea Jimmy Atupwa Jela Miaka 20

Mahakama ya Hong Kong imemhukumu bilionea na mwanaharakati maarufu wa kuunga mkono demokrasia, Jimmy Lai, kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa yanayohusiana na ukiukaji wa sheria ya usalama wa taifa, hatua ambayo imezua mjadala mkali ndani na nje ya China.

Lai, mwenye umri wa miaka 78 na raia mwenye pasipoti ya Uingereza, alikutwa na hatia ya njama ya kushirikiana na nguvu za kigeni pamoja na kuchapisha nyenzo zilizoelezwa kuwa zinahatarisha usalama wa taifa. Mahakama ilisema alitumia nafasi yake kama mmiliki wa gazeti la Apple Daily kuhimiza shinikizo la kimataifa dhidi ya Beijing na kuchochea upinzani wa kisiasa Hong Kong.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: