Mwaka 1986, Yoweri Museveni alisema wazi kuwa tatizo kubwa la Afrika ni viongozi wanaong’ang’ania madaraka kwa muda mrefu.
Miaka karibu 40 baadaye, kauli hiyo inamrudia, huku Rais huyo wa Uganda akijiandaa kuwania muhula wa saba, akiendeleza utawala wake uliodumu kwa zaidi ya miongo minne.
Museveni aliingia madarakani baada ya mapambano ya msituni yaliyoangusha tawala kadhaa, akijitambulisha kama mwanamageuzi.
Hata hivyo, katika safari ya uongozi wake, vizingiti vya kikatiba kama ukomo wa mihula na kikomo cha umri viliondolewa, hatua iliyompa nafasi ya kuendelea kutawala.
Serikali yake imekuwa ikikumbwa na tuhuma za ufisadi, ukandamizaji na udhibiti wa kisiasa, huku upinzani ukiendelea kupinga matokeo ya chaguzi, ukidai kuwepo kwa dosari na ukiukwaji wa demokrasia.
Chanzo; Cnn