Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mgawanyiko Kimataifa Athari kwa Afrika, UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameonya migawanyiko ya kimataifa jinsi ambavyo inadhoofisha juhudi za amani katika mataifa ya Afrika hasa nchini Sudan, Somalia, DR Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na eneo la Sahel.

Akizungumza mjini Addis Ababa ambapo mkutano wa 39 wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU) unafanyika, Guterres ametoa wito wa kuwepo na ufadhili unaotabirika wa kimataifa kwa ujumbe mpya wa kudumisha amani Somalia wa Umoja wa Afrika, AUSSOM.

Akizungumza katika mkutano huo unaohudhuriwa na marais na viongozi wa mataifa ya Afrika, Guterres pia alitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja nchini Sudan.

Kiongozi huyo pia amezitaka pande zinazozozana katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kuheshimu makubaliano ya amani, akisisitiza kuwa migogoro iliyokita mizizi inaendelea kuyumbisha utulivu barani Afrika. 

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: