Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

El Mencho Muuzaji Maarufu Dawa Kulevya Auawa Mexico

Nemesio Oseguera Cervantes, anayejulikana kama El Mencho, ameuawa katika operesheni kubwa ya kijeshi nchini Mexico.

Kiongozi huyo wa Jalisco New Generation Cartel alijeruhiwa vibaya wakati wa mapambano kati ya wanajeshi na wanachama wa genge lake katika jimbo la Jalisco, na alifariki alipokuwa akisafirishwa kwenda Mexico City.

Wanachama wanne wa Cartel waliuawa, huku wanajeshi watatu wakijeruhiwa. Marekani ilisaidia kwa kutoa taarifa za kijasusi.

Baada ya operesheni hiyo, wafuasi wa Cartel walichoma magari na kufunga barabara katika majimbo manane. Marekani ilikuwa imetoa zawadi ya dola milioni 15 kwa taarifa zitakazosaidia kumkamata. Serikali pia ilikamata magari ya kivita na silaha nzito.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: