Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Shambulio la Al Shabaab Lajeruhi Polisi, Vikosi Vyaimarishwa

Maafisa watatu wa Polisi nchini Kenya wamejeruhiwa vibaya baada ya gari lao la maji kukanyaga kilipuzi cha kutegwa ardhini (IED) katika eneo la Fafi, Garissa.

Shambulio hilo limetokea karibu na kambi ya wakimbizi ya Dadaab, eneo ambalo hivi karibuni vyombo vya usalama viligundua shehena ya silaha inayomilikiwa na kundi la kigaidi la Al-Shabaab linaloendesha harakati zake ndani ya kambi hiyo.

Kufuatia tukio hilo, maafisa waliojeruhiwa wamesafirishwa kwa ndege hadi jijini Nairobi kwa ajili ya matibabu maalum kutokana na hali zao kuwa mbaya.

Wakati huo huo, vikosi vya usalama vimeimarisha msako mkali katika maeneo ya mpakani na karibu na kambi hiyo ili kuwatia mbaroni waliohusika na shambulio hilo la kigaidi.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: