Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Dunia Yashtuka Ushahidi Mpya File la Eptsein

nyaraka mpya zimeibuka nchini Marekani. Nyaraka ambazo zimezua mjadala mkubwa duniani.

Baadhi ya wachunguzi sasa wanaamini kuna ushahidi unaoongezeka unaoonesha kuwa kifo cha Jeffrey Epstein huenda hakikuwa kujiua… bali mauaji yaliyopangwa. ALIUAWA!

Lakini ili kuelewa uzito wa Makala haya, lazima turudi nyuma kidogo. Jeffrey Epstein alikuwa bilionea mkubwa nchini Marekani aliyekuwa na marafiki wengi wenye nguvu duniani.

Julai 6 Mwaka 2019 alikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kufanya biashara ya ngono na unyanyasaji wa kingono wa watoto wadogo – stori ni ndefu sana kwenye hili sakata.

Akiwa bado mahabusu, Agosti 10, 2019 Epstein alikutwa amekufa katika selo yake ndani ya gereza lenye ulinzi mkali jijini New York, Marekani – ikiwa ni ndani ya mwezi mmoja tu tangu akamatwe kufunguliwa mashitaka hayo.

Serikali ilisema: alijiua kwa kutumia shuka.
Lakini tangu siku hiyo… dunia haijawahi kuamini kikamilifu stori hiyo.

Sasa, baada ya mamilioni ya kurasa za nyaraka mpya kutolewa na United States Department of Justice, maswali yanaongezeka kuliko majibu.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: