Wawakilishi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wale wa kundi la waasi la M23 wametia saini leo Jumamosi nchini Qatar, makubaliano ya mpango wa amani unaolenga kukomesha mapigano mashariki mwa Kongo.
Kuanzia mwezi Aprili mwaka huu, Qatar iliandaa na kusimamia raundi kadhaa za mazungumzo ya moja kwa moja kati ya serikali ya Kongo na waasi hao na tangu wakati huo kumekuwa kukijadiliwa masharti ya awali pamoja na kujenga mazingira ya pande hizo hasimu kuaminiana.
Pande hizo mbili zilisaini mwezi Julai tamko la kanuni ambalo halikuweka wazi namna ya kushughulikia masuala mengi muhimu ambayo ndiyo chanzo cha mzozo huo, na mwezi Oktoba hatimaye mahasimu hao walifikia makubaliano kuhusu hatua za ufuatiliaji wa kusitisha mapigano.
Chanzo; Dw