Polisi huko Mlolongo nchini Kenya, wamemkamata mwanamke kwa tuhuma za kuwapa sumu watoto wake watatu kufuatia mgogoro kati yake na mumewe.
Mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Linet Mubaba, aliwekwa chini ya ulinzi siku ya Jumanne baada ya miili ya watoto wake mapacha wa mwaka mmoja na wa miaka minne kugunduliwa nyumbani kwao.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea baada ya madai ya kutoelewana kati yake na mumewe, Alex Mogeni ambaye ni dereva.
Kwa mujibu wa polisi, mumewe anaaminika kutoroka eneo la tukio muda mfupi baada ya tukio lakini baadaye alifuatiliwa na kukamatwa.
Kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Mlolongo huku uchunguzi ukiendelea.
Miili ya watoto hao watatu imehamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City, ambako uchunguzi wa postmortem unatarajiwa kufanyika ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
Polisi wanasema uchunguzi unaendelea ili kubaini mazingira kamili ya tukio hilo, ikiwa ni pamoja na matukio yaliyosababisha mshukiwa wa kuwekewa sumu.
Chanzo; Itv