Wajumbme na baadhi ya Viongozi wameondoka ukumbini kwa njia ya maandamano ya amani wakati Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akipanda jukwaa la kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Tukio hilo la kushtua liliangazia kwa kiasi kikubwa mgawanyiko uliopo ndani ya Jumuiya ya Kimataifa kuhusu sera za Israel na mzozo unaoendelea na Ukanda wa Gaza na kuondoka kwa Wajumbe hao kumetafsiriwa kama ujumbe mzito wa kisiasa, uliotuma ishara ya wazi ya kutoridhishwa.
Licha ya maandamano hayo, Netanyahu aliendelea na hotuba yake, akitetea msimamo wa Israel na kueleza sababu za hatua zake za kiusalama.
Chanzo: Millard Ayo