Kiongozi aliyeondolewa madarakani wa Venezuela, Nicolas Maduro, alikana mashtaka yote Jumatatu mbele ya mahakama ya New York kuhusiana na biashara ya dawa za kulevya na silaha, huku akilaani vikali operesheni ya kijeshi ya Marekani iliyopelekea kukamatwa kwake.
“Mimi sina hatia, sikukubali mashtaka hayo,” alisema Maduro mwenye umri wa miaka 63 mbele ya mahakama, akiongeza kuwa alikamatwa nyumbani kwake mjini Caracas na kwamba bado anajiona kuwa rais wa Venezuela, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani vilivyokuwapo ndani ya ukumbi wa mahakama.
Chanzo; Dw