Zaidi ya watoto 100 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu kusitishwa kwa mapigano mwezi Oktoba, taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la watoto (UNICEF).Shirika hilo linaripoti kuwa wavulana 60 na wasichana 40 walio chini ya umri wa miaka 18 wamefariki dunia. Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza, inayosimamiwa na wapiganaji wa Hamas, imethibitisha takwimu hizo na mashirika ya Umoja wa Mataifa mara kwa mara yameeleza kuwa takwimu za wizara hiyo ni za kuaminika.
Chanzo; Dw