Mamlaka ya Mawasiliano Gabon imesema hatua hii inalenga kudhibiti maudhui yasiyofaa ikiwemo ya kashfa, ya chuki, na ya matusi" yalikuwa yakidhoofisha "utu, maadili ya umma, heshima ya raia, mshikamano wa kijamii, utulivu wa taasisi za Jamhuri na usalama wa taifa.
Mamlaka hiyo imeongeza kuwa "kuenea kwa taarifa za uongo", "unyanyasaji mtandaoni" na "ufichuzi wa data binafsi bila idhini" ni miongoni mwa sababu za uamuzi huo. Hata hivyo, serikali imesema uhuru wa kujieleza bado ni haki ya kikatiba.
Wakati huo, serikali ya Rais Brice Oligui Nguema inakabiliwa na migomo ya walimu na vitisho vipya kutoka sekta ya afya, ishara ya msukosuko unaoendelea nchini nchini humo.
Chanzo; Dw