Maandamano hayo yaliyoratibiwa na viajana kupitia mitandao ya kijamii yameishutumu serikali kwa kupuuza huduma muhimu ikiwemo elimu na afya, badala yake fedha kuwekezwa katika maandalizi ya Kombe la Dunia 2030.
Tayari polisi imeingilia kati maandamano hayo na kuwakamata baadhi ya vijana wanaodaiwa kuchochea maandamano hayo chini ya kundi la GEN Z 212.
Serikali imesema iko tayari kufanya mazungumzo ya kitaifa na vijana kujadili njia ya kushughulikia matwakwa yao.
Chanzo: Dw