Zaidi ya watu 70 wameuawa katika shambulizi la Droni linalodaiwa kufanywa na wanamgambo wa RSF kwenye Msikiti mmoja huko al-Fashir, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini siku ya Ijumaa.
Shambulizi hilo limetokea wakati vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe vikiingia mwaka wa tatu kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF. Umoja wa Mataifa umedokeza kwamba ukatili unazidi kuongezeka katika mzozo huo siku baada ya siku.
Chanzo; Dw