Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Uchunguzi Kifo cha Mtoto wa Gaddafi Waanza

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa Libya, Muammar Gaddafi, Saif al-Islam, anatarajiwa kuzikwa leo Ijumaa, Februari 6, 2026 katika mji wa Bani Walid, ulioko magharibi mwa nchi hiyo na unaotajwa kuwa ngome ya watiifu wa familia ya Gaddafi.

Saif al-Islam aliuawa Februari 3, 2026 baada ya kushambuliwa na watu wanne wenye silaha nyumbani kwake kaskazini magharibi mwa mji wa Zintan.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya ndani ya Al-Wasat, mwili wake uliwasili Bani Walid jana kabla ya mazishi na kupokewa na kundi la waombolezaji.

Wakati wa utawala wa zaidi ya miongo minne wa baba yake, Saif al-Islam aliwahi kuonekana kama mrithi mkuu wa kisiasa. Mwaka 2021 alijitokeza tena katika siasa kwa kugombea urais, lakini uchaguzi huo haukufanyika.

Mamlaka yenye makao yake Tripoli imeamuru kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu mauaji hayo na kutoa salamu za rambirambi, huku viongozi wa upande wa mashariki wa nchi hiyo, ambao ni hasimu wa kisiasa, wakiwa bado hawajatoa tamko rasmi.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: