Mwili wa Mtanzania Joshua Mollel, aliyeuawa na kundi la Hamas nchini Israel miaka miwili iliyopita, unatarajiwa kuwasili kesho katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ukitokea Tel Aviv, Israel. Mollel alikuwa nchini humo akifanya mafunzo ya kilimo katika eneo la Kusini mwa Israel.
Leo, Ubalozi wa Tanzania nchini Israel uliandaa ibada maalumu ya kumuaga marehemu kabla ya safari ya kurejeshwa nchini.
Israel imekabidhi jumla ya miili 285 ya Wapalestina kwa upande wa Palestina, ikiwa ni sehemu ya makubaliano yaliyowezesha kupokelewa kwa miili ya mateka 19 Waisraeli waliorejeshwa na Hamas, pamoja na miili ya mateka watatu raia wa kigeni,raia mmoja wa Thailand, mmoja wa Nepal na Mtanzania mmoja.
Chanzo; Bbc