Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema hakuna tatizo kwa Serikali ya nchi hiyo kuzima mtandao kwa kuwa wao ndio walioutengeneza na hivyo pale wanapoona inafaa hawana budi kuuzima.
Amesema hayo katika mahojiano yake na chombo kimoja cha kimataifa wakati huu ambapo kura zinaendelea kuhesabiwa huku akielezwa kuongoza dhidi ya mpinzani wake Robert Kyagulanyi (BobiWine).
"Sisi ndio tulioujenga huo mtandao ambao wewe unauzungumzia kwahiyo kuuzima ni kwasababu ya kushughulika na wahalifu wanaotaka kutuharibia nchi" amesema Museveni.
Tume ya Uchaguzi Uganda inaendelea kupokea matokeo ya uchaguzi uliofanyika jana Alhamisi kutoka vituo mbali mbali vya kupiga kura ambapo matokeo ya awali yaliyotangazwa yanaonesha kuwa Museveni amepata asilimia 76.25 ya kura zilizohesabiwa kufikia sasa kulingana na hesabu kutoka karibu nusu ya vituo vya kupigia kura.
Chanzo; Nipashe