Wanasiasa wa Marekani wameionya Uingereza na washirika wake wengine dhidi ya kuitambua Palestina kama dola huru, wakisema hatua hiyo itawapa nguvu wanamgambo wa Hamas na kutishia usalama wa Israel.
Wanasiasa hao wa chama cha Republican akiwemo mbunge wa New York Elise Stefanik na Seneta Rick Scott, wameyatumia barua mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Canada na Ausrealia pamoja na washirika wengine muhimu, wakiwataka kupinga juhudi katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa za kuihalalisha na kuitambua Palestina kama dola huru.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatarajiwa kutangaza rasmi uamuzi wa nchi yake kuitambua Palestina kesho Jumapili
Chanzo; Dw