Kumalizika kwa mkataba wa New START kumefikisha mwisho makubaliano yaliyosalia ya udhibiti wa silaha za nyuklia kati ya Marekani na Urusi.
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa wito wa mkataba mpya wa nyuklia kuandaliwa badala ya kuongeza muda wa uliokuwepo.
Saa chache baada ya muda wa mkataba uliodhibiti silaha za nyuklia za nchi mbili zenye hazina kubwa zaidi duniani (Marekani na Urusi) kwa zaidi ya miongo miwili kuisha, Trump alisema kuwa mkataba wa New START "ulijadiliwa vibaya" na "unakiukwa vibaya sana."
Trump amewataka wataalamu kufanyia kazi mkataba mpya wa Nyuklia ambao utadumu kwa muda mrefu na uwe bora na wa kisasa.
Chanzo; Dw