Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Watu Zaidi ya 900,000 Wahaamishwa Ufilipino

Zaidi ya watu 900,000 wamehamishwa nchini Ufilipino kabla ya Kimbunga Fung-wong, ambacho kinatarajiwa kutua nchini humo jioni ya leo, Jumapili, Novemba 9, 2025.

Kimbunga hicho kimepandishwa hadhi na kuwa kimbunga kikuu (super typhoon) chenye kasi ya upepo wa wastani wa kilomita 185 kwa saa na vipindi vya upepo mkali vinavyofikia hadi kilomita 230 kwa saa, kwa mujibu wa Idara ya Hali ya Hewa ya Taifa ya nchi hiyo.

Mkoa wa Mashariki wa Bicol ndiyo ulikuwa wa kwanza kupigwa moja kwa moja na kimbunga hicho Jumapili asubuhi, huku kisiwa cha Luzon ambacho ndicho kitovu cha makazi ya watu wengi nchini humo — kikitarajiwa kuathiriwa kufikia Jumapili usiku.

Fung-wong, kinachojulikana kitaifa kama Uwan, kimekuja siku chache tu baada ya kimbunga kingine, Kalmaegi, kuleta uharibifu mkubwa na kusababisha vifo vya takribani watu 200.

Shule kadhaa zimefuta masomo ya Jumatatu au kuhamishia masomo hayo mtandaoni, huku takribani safari za ndege 300 zikifutwa.

Inatarajiwa kwamba Fung-wong kitadhoofika baada ya kutua kati ya maeneo ya Baler na Casiguran, ingawa kitaendelea kubaki kuwa kimbunga kikali kadri kinavyosonga juu ya kisiwa cha Luzon.

Zaidi ya milimita 200 za mvua zinatarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo ya Luzon, na kati ya milimita 100 hadi 200 katika eneo la Metro Manila.

Mvua hizo zinatarajiwa kusababisha mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi.

Maeneo ya Mashariki mwa Ufilipino tayari yameanza kushuhudia mvua kubwa na upepo mkali, kwa mujibu wa afisa wa hali ya hewa aliyetoa taarifa Jumamosi jioni.

Ingawa sehemu kubwa ya nchi inatarajiwa kuathiriwa, kuna wasiwasi maalum kuhusu maeneo yatakayopigwa moja kwa moja, ikiwemo Kisiwa cha Catanduanes, kilichopo Mashariki mwa Mkoa wa Bicol, ambako hali mbaya sana ya hewa imeripotiwa mapema Jumapili asubuhi.

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: