Gereza la Alcatraz, maarufu kama 'The Rock', ni miongoni mwa magereza yenye ulizi mkali zaidi kuwahi kuwepo duniani.
Lilijengwa juu ya kisiwa kidogo chenye miamba mikali katikati ya Ghuba ya San Francisco, Marekani.
Kuanzia mwaka 1934 hadi 1963, gereza hili lilitumika kuwafungia wafungwa hatari zaidi na waliokuwa wakitoroka magereza mengine kwa urahisi.
Mfumo wa Ulinzi wa Gereza la Alcatraz
Alcatraz halikuhitaji kuta nene sana au askari wengi kupita kiasi; mazingira yenyewe yalikuwa ulinzi mkuu.
Gereza la Alcatraz lilikuwa mahali ambapo muda haukupita, ulibaki umesimama. Kila siku ilifanana na nyingine: mlango wa chuma ukifunguliwa, hesabu ya wafungwa, ukimya, baridi, na sauti ya bahari ikigonga miamba kwa hasira.
Ndani ya mazingira haya ndipo Frank Morris, John na Clarence Anglin walianza kitu ambacho hata wao wenyewe hawakujua kama kingewezekana.
Hakukuwa na mpango wa haraka. Hapakuwa na ramani. Kulikuwa na swali moja tu kichwani mwao: “Je, kuna ufa wowote kwenye mfumo huu?”
Morris alikuwa mtu wa kuchunguza. Siyo mtu wa hasira, bali wa macho makali. Aligundua kuwa ukuta wa seli yake haukuwa mgumu kama alivyoamini. Haukupasuka kwa makonde, lakini ulionnesha dalili za kuchoka.
Bahari ilikuwa imefanya kazi yake kwa miongo kadhaa, unyevu ukiila saruji polepole, kimya kimya.
Hapo ndipo akili ilipoanza kufanya kazi.
Sio “tutoroke leo.”
Chanzo; Global Publishers