Mwanaume mmoja nchini Marekani, Jonathan Gerlach (34) amekamatwa na kushtakiwa kwa makosa zaidi ya 300 yakihusisha wizi wa zaidi ya Mafuvu 100 ya Binadamu pamoja na vito vya thamani vilivyoibwa katika Makaburi ambapo tukio hilo limeripotiwa kutokea katika Makaburi ya Mount Moriah mjini Philadelphia.
Kwa mujibu wa Polisi wa Jiji la Philadelphia kukamatwa kwa Jonathan kunatokana na uchunguzi wa uvamizi na wizi wa vito vya thamani katika Makaburi hayo na Polisi wamesema wakati wa upekuzi katika Nyumba yake walikuta mifupa ya Binadamu ikiwemo mikono na miguu iliyokaushwa pamoja na miili iliyooza iliyokuwa imehifadhiwa kwenye stoo ya Nyumba hiyo.
Hadi sasa Polisi wamesema haijabainika sababu ya Mtuhumiwa kukusanya na kuhifadhi mabaki hayo ya miili pamoja na vito vya thamani ila uchunguzi wa kina unaendelea huku Jonathan Gerlach akitarajiwa kufikishwa Mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.
Chanzo; Millard Ayo