Akizungumza na The Citizen Tanzania, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andy Lentz amesema mchakato wa kuweka wazi tukio la kukamatwa kwa raia wa Marekani kwenye Vyombo vya Habari ni “jambo la kusikitisha” na “lisilofaa.”
Amesema tukio hilo limekuzwa kupita kiasi na baadhi ya viongozi wa Serikali, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu faragha ya raia wa Marekani.
Jeshi la Polisi lilisema kuwa mabomu hayo ni silaha ambazo hata kama Mtuhumiwa angeomba kibali, asingeruhusiwa kuingia nazo nchini kwa mujibu wa Sheria za Tanzania.
Chanzo; Jamii Forums