Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Marekani Kususa Mkutano wa G-20 Afrika Kusini Kisa Ubaguzi wa Rangi

Donald Trump amesema Marekani haitahudhuria mkutano wa kilele wa G20 nchini Afrika Kusini kutokana na madai yaliyokanushwa kuwa Wazungu wanateswa nchini humo.

Rais wa Marekani alisema ni "aibu kubwa" kwamba Afrika Kusini ni mwenyeji wa mkutano huo, ambapo viongozi kutoka mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi duniani watakusanyika mjini Johannesburg baadaye mwezi huu.

Wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini ilielezea uamuzi wa Ikulu ya White House kuwa "wa kusikitisha", wakati msemaji wa wizara ya mambo ya nje, Chrispin Phiri, aliiambia BBC kwamba mafanikio ya mkutano huo "hayatategemea nchi moja mwanachama".

Hakuna chama chochote cha kisiasa nchini Afrika Kusini kinachodai kuwa kuna mauaji ya halaiki nchini Afrika Kusini.

Akiongea na kipindi cha Newshour, Bw Phiri alisema kuwa Trump "anapanga mgogoro ... kwa kutumia historia chungu ya ukoloni wa Afrika Kusini". Pia alisema "hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa Wazungua wanateswa nchini Afrika Kusini", na kuongeza: "Afrika Kusini ina matatizo yake na tunayashughulikia. Nadhani uhalifu unaathiri kila mtu, bila kujali jamii fulani."

"Tutaendelea bila Marekani," alisema, Bw Phiri .

Trump aliweka ujumbe kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social akisema: "Ni aibu kubwa kwamba G20 itafanyika Afrika Kusini. "Waafrikana (watu waliotokana na walowezi wa Uholanzi, na pia wahamiaji wa Ufaransa na Wajerumani) wanauawa na mashamba yao yananyakuliwa kinyume cha sheria," aliandika.

 

Chanzo; Bbc

Kuhusiana na mada hii: