Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Aliyejaribu Kuanzisha Nchi Yake Afungwa Kifungo cha Maisha Mara 4

Mahakama nchini Nigeria imemkuta na hatia ya ugaidi na mashtaka mengine kiongozi wa vuguvugu la kujitenga, Nnamdi Kanu kutokana na kesi iliyoendeshwa kwa zaidi ya miaka kumi.

Kiongozi huyo amehukumiwa kifungo cha maisha mara nne, pamoja na vifungo vingine vitakavyotumikiwa kwa pamoja.

Jana, Alhamisi Novemba 20, 2025 ulinzi uliimarisha maeneo ya jengo la mahakama katika mji mkuu, Abuja, kabla ya hukumu kutolewa iwapo kungetokea maandamano kutoka kwa wafuasi wa Kanu.

Upande wa mashtaka ulikuwa umetaka itolewe adhabu ya kifo, lakini Jaji James Omotosho amesema kwamba kwa mtazamo wa nchini humo sasa adhabu ya kunyonga haitatolewa badala yake atatumikia adhabu mbadala.

Katika uamuzi wake, amesema ameridhika kwamba Kanu alifanya matangazo kadhaa yaliyochochea vurugu na mauaji kama sehemu ya kampeni yake ya kutaka kuanzisha taifa tofauti kusini mashariki mwa Nigeria, linalojulikana kama Biafra.

Tovuti ya BBC imeeleza kwamba, Kanu alipatikana na hatia katika mashtaka yote saba aliyokabiliwa nayo. Mbali na ugaidi, mashtaka hayo yalijumuisha uhaini na ushiriki katika harakati iliyopigwa marufuku.

Kanu amekuwa akikana mashtaka hayo kila wakati na alipinga mamlaka ya mahakama. Mwanzoni mwa kesi, aliwafukuza mawakili wake lakini alikataa kujitetea.

Hakuwa mahakamani wakati hukumu inatolewa, baada ya kuondolewa kutokana na tabia isiyodhibitika.

Akiwa mtu ambaye hapo awali hakujulikana sana, alijipatia umaarufu kitaifa mwaka 2009 alipoanzisha Radio Biafra, kituo kilichokuwa kikitoa wito wa kuanzishwa kwa taifa huru la watu wa Igbo, kikirusha matangazo yake kuelekea Nigeria kutoka London.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: