Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mgomo Kupinga Sera za Trump Wafanyika Marekani

Waandamanaji waliendesha mgomo wa “hakuna kazi, hakuna shule, hakuna ununuzi” kote Marekani kupinga msako wa wahamiaji unaofanywa na utawala wa Trump.

Baadhi ya shule huko Arizona, Colorado na majimbo mengine zilifuta masomo mapema jana Ijumaa kwa kutarajia wanafunzi wengi kutohudhuria.

Maandamano hayo, yanafanyika huku kukiwa na hasira kubwa kufuatia mauaji ya Alex Pretti, muuguzi wa wagonjwa mahututi ambaye alipigwa risasi mara kadhaa baada ya kutumia simu yake kurekodi maafisa wa Ulinzi wa Mpaka wakifanya operesheni ya kuwakamata wahamiaji mjini Minneapolis.

Kifo hicho kimeongeza ukosoaji kuhusu mbinu za utawala wa Trump, kufuatia kifo cha Januari 7 cha Renee Good, aliyepigwa risasi na afisa wa Uhamiaji na Forodha (ICE) wakati akiwa ndani ya gari lake.

 

 

Chanzo; Dw

Kuhusiana na mada hii: