Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Serikari ya Marekani Yafungwa, Mvutano Mkali wa Vyama kisa Bajeti

Serikali ya Marekani imefungwa rasmi baada ya Chama cha Republican cha Rais Donald Trump na chama cha upinzani cha Democrat kushindwa kufikia makubaliano juu ya mswada muhimu wa matumizi ya serikali.

Shutdown hii, ambayo ilianza saa 6 usiku kwa saa za Afrika Mashariki Jumatano, ni ya kwanza kwa Marekani katika kipindi cha karibu miaka saba. Hatua hii imewalazimisha mamia ya maelfu ya wafanyakazi wa serikali kwenda likizo bila malipo na imeweka huduma nyingi muhimu za umma hatarini – kutoka tafiti za afya hadi hifadhi za taifa.

Chanzo cha mvutano ni ufadhili wa huduma za afya. Democrats wamekataa kuunga mkono mpango wa Republicans ambao wanasema utawafanya mamilioni ya Wamarekani washindwe kumudu bima ya afya. Wanataka ruzuku zinazosaidia wananchi kupata bima ya afya ziendelee na kupinga kupunguzwa kwa huduma za Medicaid zilizofanywa na utawala wa Trump.

Republicans, ingawa wanadhibiti mabunge yote mawili, hawana kura 60 zinazohitajika kupitisha mswada huo katika Seneti. Trump kwa upande wake ameashiria kuwa yupo tayari kwa shutdown ya muda mrefu – na hata amependekeza inaweza kutumika kama nafasi ya kupunguza idadi ya wafanyakazi wa serikali.

Vyama vyote viwili sasa vinatafutana lawama. Republicans wanasema Democrats wataadhibiwa na wapiga kura kwa “kufunga” serikali, huku Democrats wakisisitiza mapambano yao ya kulinda huduma nafuu za afya ni ya haki na yanayoungwa mkono na wananchi.

Kwa sasa, Marekani iko katika hali ya sintofahamu – serikali ikiwa imefungwa, na maisha ya wananchi milioni kadhaa yakibebwa na mvutano wa kisiasa.

 

Chanzo: Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: