Kundi la waasi wa AFC/M23, leo Alhamisi tarehe 8 Januari 2026, limeendesha shughuli za mazishi ya watu 22 waliopoteza maisha kufuatia mashambulizi ya droni yanayodaiwa kufanywa na jeshi la serikali ya Kinshasa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Waasi hao, ambao wamekuwa wakitajwa kuungwa mkono na Rwanda, wameelekeza lawama kwa serikali ya Rais Félix Tshisekedi, wakidai mashambulizi hayo yamelenga maeneo yanayokaliwa na raia katika maeneo yanayodhibitiwa na M23.
Kwa mujibu wa taarifa za AFC/M23, tukio la hivi karibuni lilitokea tarehe 2 Januari 2026 katika mji wa Masisi, mkoa wa Kivu Kaskazini, ambapo shambulizi la droni lilisababisha vifo vya watu sita na kujeruhi wengine zaidi ya ishirini.
Mashambulizi hayo yamezidisha mvutano unaoendelea mashariki mwa Congo, huku pande husika zikiendelea kurushiana lawama kuhusu usalama wa raia katika maeneo ya mapigano.
Chanzo; Cnn