Kijana mmoja Eric (sio jina lake halisi) amejikuta akipatwa na mshangao mkubwa baada ya kushuhudia video ikisambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha yeye pamoja na mpenzi wake wakishiriki tendo la ndoa, jambo lililofanyika bila wao kujua.
Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa mwaka 2023, wakati wawili hao wakiwa mapumzikoni katika hoteli moja mjini Shenzhen kusini mwa China, bila kujua kwamba walikuwa wanachunguzwa na kurekodiwa.
Ilielezwa kuwa Eric ambae ni mfuatiliaji wa mitandao inayochapisha picha/video za ngono, wakati akiendelea kutazama video mojawapo aligundua kwamba watu aliokuwa akiwatazama wakiingia chumbani kujipumzisha na kushiriki tendo la ndoa kumbe ilikuwa ni yeye na mpenzi wake.
Pia ilielezwa kuwa vitendo vyao vya kushiriki ngono vilirekodiwa na kamera za siri ambazo zilifichwa kwenye chumba walicholala. Na baadaye picha hizo za video zilichapishwa kwenye mitandao na kutazamwa na maelfu ya watu kwenye ukurasa wa mtandao wa kuchapisha video za ngono ambao yeye mwenyewe Eric alikuwa anapenda kuutazama.
Biashara haramu ya picha za ngono zilizorekodiwa kwa siri almaarufu SPY CAM imekuwepo nchini China kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, japo kurekodi na kutayarisha picha hizo za video kumeharamishwa na ni kinyue na sheria nchini humo.
Mwezi Aprili mwaka jana, kanuni mpya za serikali zilizotolewa, na kwamba sheria hizo ziliwataka wamiliki wa hoteli kukagua vyumba vya kulała kwa ajili ya kupata na kuondoa kamera za siri.
Chanzo; Nipashe